Wednesday, December 12, 2007

Leo nimesikika BBC Kiswahili

Posted by Mlenge in 17:44:10 | Permalink | Comments (3)

Sunday, December 2, 2007

Mwisho wa Tanzania (1964 - 2025): Visababishi

Taifa la Tanzania, kwa hiari ya wale wanaoitawala, limesaini mkataba wa EAC ambao unahitimisha kuwepo kwa taifa hilo ifikapo mwaka 2025.

Kwa maoni yangu binafsi, sababu zifuatazo ndizo zilizopelekea kuhitimishwa “kilaini” uhai wa taifa la Tanzania:

1. Dhana kwamba watawala wamechukua nafasi ya wakoloni na kwamba wananchi wengine tunatakiwa kuendelea kuwa watawaliwa sawa tu na wakati wa ukoloni. Yaani watawala wamekuwa wakoloni-weusi, na wananchi tumeendelea kuwa watawaliwa tu. Tofauti na wakoloni wazungu waliokuwa wanawajibika kwa Malkia, wakoloni-weusi hawana wanayewajibika kwaye. [wananchi wamekataa EAF/EAC, lakini watawala wanaendelea na mradi wao bila kujali].

2. Kutojiamini kwamba watawala hao wanaweza kutawala ‘vizuri kama vile tu wazungu’. Hivyo muda mwingi kuutumia kutaka kusifiwa na Wazungu kwamba ‘kumbe wakoloni weusi nao wanajua kutawala’. Kwa kuwa EAC ni wazo la wazungu, lazima likubaliwe tu.

3. Nani anajali?

Posted by Mlenge in 19:47:01 | Permalink | No Comments »

Tanzania (1964 - 2025) — Death of a Nation

Mwisho wa hadithi!

Tanzania itakuwa historia!

Kwa mujibu wa taarifa, Tanzania imesaini mkataba wa EPA chini ya kimvuli cha EAC (http://www.ippmedia.com/ipp/observer/2007/12/02/103464.html) . EPA ndiyo ilikuwa njia pekee yenye matumaini iliyobakia ya kuinusuru Tanzania. Kama Tanzania ingesaini mkataba wa EPA kupitia SADC, basi ingekuwa ndiyo salama yake, kwa vile ungefika muda Tanzania ingelazimika kutoka EAC. Kwa sasa, mkataba wa EPA ndiyo mwisho wa Tanzania kuwemo SADC. Labda kama itasaini pia kupitia SADC, jambo ambalo ni mashaka iwapo linawezekana.

Vinginevyo, Tanzania inahitaji sasa hivi watawala wenye dira na mwelekeo wa kuimarisha uhuru na umoja wa Tanzania utakaodumu zaidi ya miaka hamsini ijayo. With all due respect (Wazungu husema), sidhani kama wale wanaotawala nchi ya Tanzania wana dira na mwelekeo wa kuwa na nchi huru ya Jamhuri ya Tanzania ifikapo mwaka 2050. Watawala tulionao ndio wale waliosaini mikataba ya EAC ambayo dira na mwelekeo wake ni kufuta Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haraka iwezekanavyo.

Na kwa hatua EAC iliyofikia sasa, itabidi kuwa na watawala wenye maono, dira na mwelekeo tofauti na wale waliopo sasa hivi madarakani ili kuweza kulinasua taifa la Tanzania toka mdomoni mwa ‘mamba’ EAC.

Kwa sasa ni wakati wa kurekodi hali ilivyo wakati nchi inaelekea mwisho wake uliobarikiwa na watawala wa Tanzania.

Tanzania (1964 - 2025) itakumbukwa kwa wema wa mshumaa (kuangazia wengine huku wenyewe ukiteketea), ngonjera za “amani na mshikamano” pamoja na maradhi ya kupenda misifa bila kuzingatia tija.

Posted by Mlenge in 19:35:18 | Permalink | No Comments »